Main
Mzalendo Kimathi Edition: Chapa ya pili
Mzalendo Kimathi Edition: Chapa ya pili
Mîcere Gîthae Mũgo; Ngũgĩ wa Thiong'o; Raphael Kahaso
5.0
/
5.0
0 comments
"Yamesemwa na kuandikwa mengi juu ya kiini cha mapambano ya Mau Mau na vikosi vya Wakoloni Waingereza. Lakini je, kiini hiki kimezungumziwa vya kutosha katika fasihi ya Kenya? Ni kwa nini fasihi hii imewadunisha wazalendo na kuwafanya wasioweza kuiunda historia yao? Kwa nini waimbaji wetu Kenya hawajapata kuimba nyimbo za kuwasifu mashujaa kama Dedan Kimathi na ujasiri wao? Historia na matendo waliyoyaandika wanahistoria na waandishi wengine ni vya nani? Haya ni baadhi tu ya maswali yaliyowafanya Ngugi wa Thiong'o na Micere Githae Mugo kuuandika mchezo wa Mzalendo Kimathi, mchezo wa aina ya pekee unaoonyesha mapambano ya Kenya katika kujikomboa. Mhusika mkuu ni Kimathi, kiongozi shupavu wa mapinduzi ya Mau Mau. Ingawa anateswa kwa njia nyingi, Kimathi anagoma kabisa kujisalitisha na Ubeberu wa Waingereza."
Comments of this book
There are no comments yet.