Main Imân na Uislam

Imân na Uislam

4.0 / 5.0
0 comments
Toleo la Kituruki lilitolewa na Huseyn Hilmi Isik KUMBUKA Mwandishi wa kitabu I’tiqad-nama, Mawlana Diya’ad-din Khalid al Baghdadi al-Uthman (alizaliwa mwaka 1192 hijiri sawa na 1778 miladi katika mji wa Shahrazur kaskazini mwa Baghdad, na alifariki dunia mwaka 1242 hijiri sawa na 1826 katika mji wa Damascus (syria) quddisa sirruh), Aliitwa Uthman kwasababu anatokana na ukoo wa Uthman Dhu’nurain radiya-Allahu ta’ala anh ambaye ni khalifa wa tatu. Alipokuwa anamfundisha ndugu yake Hadrat Mawlana Mahmud Sahib hadith ambayo ni maarufu sana kama Hadith al-Jibril, na ndio ya pili ndani ya kitabu Al-ahadith al-arba’un zilizotolewa na mwanachuoni marufu an-Nawawi, Hadrat Sahib alimuomba kaka yake mkubwa kuifafanua zaidi hadith hiyo. Mawlana Khalid, ili kuridhisha moyo wa mdogo wake na kutimiza ombi lake alikubali kufafanua hadith as-sharifu hiyo na akatunga kitabu kwa lugha ya ki faris kwa jina la I’tiqad-nama. Tafsiir yake kwa lugha ya kituruki kinaitwa “Herkese Lazim Olan Iman”, na pia kilitafsiriwa kwa lugha ya kingereza na kuitwa Belief and Islam, Kifaransa (Foi et Islam) na Kijerumani (Glaube und Islam) mwaka 1969, na baadae kikatafsiriwa katika lugha mbali mbali kama: Kitamil, Kiyoruba, Kihausa, Kimalayalam na Kidanish. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Awabariki vijana wetu wasio na hatia kwa kusoma na kujifunza i’tiqad sahihi (iman) kama ilivyo fikishwa na wana vyuoni wa Ahhl as-Sunna. ____________________ Kumbusho la mchapishaji: Yeyote anayetamani kuchapisha kitabu hiki kwa nakala yake asili au kitafsiri kwa lugha nyengine anaruhusiwa kufanya hivyo; pia na watu wanaofanikisha manufaa ya tendo kubwa hili wanapewa vibali kupata baraka ambazo badae tunaziendeleza mbele ya Mwenyezi Mungu kwa majina yao pia shukuran zetu na tunawashukuru sana. Hata hivyo, ruhusa inategemea na hali ya karatasi hutumika wakati wa kuchapisha kwani ni lazima ziwe nzuri na ubunifu wake uwe mzuri na mandishi yawe yamewekwa vizuri bila makosa yeyote. ____________________ Tahadhari: wamisionari wanafanya juhudi kubwa kutangaza Ukrisito; Wayahudi nao wanafanya bidi kusambaza Talmudi; na Hakikat Kitabevi (hifadhi ya vitabu) Istanbul wanapambana kutangaza Uislamu; ma freemason wanafanya jitihada za kuangamiza dini. Mtu mwenye busara, elimu na fahamu atafahamu na atafata moja ya hizo njia ilio ya ukweli na atasaidia kusambaza wokovu huo kwa binadamu wote. Hakuna njia bora zaidi na ya thamani kwa kuwahudumia binadamu kuliko kufanya hivyo. “Subhan-Allahi wa bi-hamdihi subhan-Allahil-adhim.” Dua hii inayitwa Kalima-i-tenzih, ikitajwa na mtu kila asubuhi mara mia moja(100x) na jioni pia kwa idadi hiyo hiyo, inamfanya mtu kusamehewa madhambi yake na inamfanya pia kulindwa dhidi ya kutenda maovu tena. Dua hii pia imenukuliwa kutoka kwenye barua ya mia tatu na saba (307) na mia tatu na nane (308) katika juzuu ya kwanza kwenye kitabu kinachoitwa Maktubat kilichoandikwa na Walii pia mwanachuoni mkubwa Imam Rabbani quddisa sirruh vile vile kwenye toleo la kituruki. Ya Rahman, ya Rahim, ya afuwwu ya Kerim. Lengo la Hakikat Kitabevi (hifadhi la vitabu tukufu linalopatikana Fatih, Istanbul) ni kuelimisha imani yetu, Uislamu na kufanya nchi yetu iliobarikiwa kupendwa na watu ulimwenguni. Tunaomba Mwenyezi Mungu awe radhi na watu wanaotusaidia! Amin. Mpenzi msomaji, Assalamu alaikum warahmatullahi wabaraqaatuh. Mandishi yote ndani ya kitabu hiki yamenukuliwa kutoka kwenye vitabu vilivyo andikwa na wanavuoni waisilamu. Hatujaongeza kitu chochote kwenye nakala hizi. Tumefanya kazi hi ambayo ni muhimu sana kwa madhumuni maradufu, kutumikia watu na pia kutambulishwa kutoka kwenye watu wanao fanya kazi kwa lengo la kufanya watu wafurahie maisha yao na wale wanaopigania au wanaolinda haki za binadamu. Unaposoma – 3 – mandishi ya hawa wanaviuoni wakubwa ulimwenguni kote kwa uangalifu na kuyatilia maanaani, hupata elimu yenye manufaa Insha-Allahu ta’ala. Tunaeneza Salamu zetu na upendo wetu kwenu. Tunaomba Mwenyezi Mungu awabariki na afya njema na maisha marefu yenye matunda! Amin. Wa sall-Allahu ala Sayyidina Muhammadin wa ala Al-i- Muhammadi wa barik ala Sayyidina Muhammadiin wa ala Al-i- Muhammadi. Allahumma Rabbana atina fi-d-dunia hasanatan wafil- akhirat-i-hasanatan wa qina adhab-an-nar bi-rahmatika ya Arhamur- Rahimiin! Amiin. Hakikat Kitabevi
Request Code : ZLIBIO2175894
Categories:
Year:
2016
Publisher:
Hakikat Kitabevi Publications
Language:
Swahili
Pages:
112

Comments of this book

There are no comments yet.